2016-10-30-PHOTO-00000146

Waziri Mwijage azindua mashine ya kusaga nafaka kijijini Maisha Plus

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa nchini Tanzania Mhe. Charles Mwijage leo amezindua rasmi mashine ya kusaga na kukoboa nafaka katika kijiji cha Maisha Plus.

Akizungumza  wakati wa uzinduzi wa mashine hiyo Mhe. Mwijage alisema kitendo cha washiriki hao 16 kutoka nchi tano za Afrika Mashariki kuweza kubuni mashine ni sawa na kufaulu mitihani mikubwa ya kimaisha.

Alisema mashine hiyo ni mkombozi kwa watu wote wa Afrika Mashariki kwa sababu inaweza kusaga bila kutumia umeme lakini pia inamuwezesha mtu kufanya mazoezi.

2016-10-30-PHOTO-00000145

“Hii mashine ni njia mbadala ya kumuwezesha mtu kufanya mazoezi badala ya kwenda gym kufanya mazoezi utaweza kutumia mashine hii ukiwa unasaga nafaka huku unafanya mazoezi,” alisema Mwijage.

2016-10-30-PHOTO-00000148

Alisema ni vyema kwa washiriki kutumia njia hiyo  kuweza kubuni mashine nyingine zaidi ili kuweza kuongeza soko la Afrika Mashariki.

Alitoa wito kwa mshiriki atakayeshinda Tzshs. Milioni 30 za Maisha Plus aziwekeze katika uchumi wa viwanda.

2016-10-30-PHOTO-00000147

Grace PEMBA kutoka Mtwara aula

Katika hatua nyingine, Waziri Mwijage ameahidi kumpatia mshiriki Grace Pemba kutoka Mtwara mashine ya kubangua korosho yenye thamani ya shilingi milioni nane.

“Ukienda ripoti SIDO Mtwara, waambie Waziri amesema mnipe mashine ya kubangua korosho.”

Grace aliyekua anafanya kazi katika saluni za kutengeneza nywele ameshauriwa kutumia mashine hiyo kujikwamua kiuchumi.

Vipindi vya Maisha Plus vinarushwa na kituo cha Televisheni cha Azam Two na pia kupitia akaunti ya Youtube ya Maisha Plus. Taarifa zaidi kuhusu mashindano hayo zinapatikana katika tovuti rasmi ya www.maishaplus.tv na kupitia mitandao ya Maisha Plus ya Facebook, Instagram na Twitter.

Maisha Plus inaratibiwa na kampuni ya DMB na vipindi kutengenezwa na kampuni za True Vision Productions, KP Media na Pumzika Communications.

#VijanaNdioNgazi #HapaKaziTu