Washiriki wa Maisha Plus wakiingia kijijini

Kijiji cha Maisha Plus chafunguliwa rasmi – Washiriki watakiwa kujijengea nyumba

Kijiji cha Maisha Plus kimefunguliwa rasmi. Washiriki 29 kutoka nchi 5 za Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda wameingia kijijini kuanza safari ya wiki nane kuwania Tzshs. Milioni 30.

Wafuatao wameingia kijijini: 

Burundi: Kamo Daniel, Nibigira Baswari, Ngenda Pili, Khalid Said

Kenya: Alex Esau, Mike Curtywer, Olive Kiarie, Deniace Machocho

Rwanda: Bingo Regis, Gakumba Patrick, Karekezi Jean, Umubyeyi Solange

Tanzania:  Paniely T. Mollel, Yasinta Mrisho (Arusha), Irene Ishengoma, Faisal Moshi (Dar Es Salaam), Aloyce A. Sambuta, Kachen E. Kabobo (Dodoma), Rodha Mgaya (Iringa), Salmin Omary, Tamasha Kyamba (Mbeya), Asedi Clemence, Fodrick Mapunda (Mwanza), Grace Pemba (Mtwara), Ally Khatibu Ally, Rukia S. Athuman (Zanzibar)

Uganda: Assimwe M. Mutekanga, Kankunda S. Titi, Namita Cherie

 Ally Masoud  maarufu kwa jina la Kipanya akiwa katika kijiji na Babu mwenyeji wa kijiji cha Maisha Plus wakijadili jambo wakati wakiwangoja washiriki wa shindano hilo.
 Babu mwenyeji wa kijiji cha Maisha Plus akiwa anajivinjali kijijini hapo
 Haya ni baadhi ya maeneo katika kijiji cha Maisha Plus ambapo washiriki hao kutoka Nchi Tano za Afrika Mashariki watakaa kwa wiki 8
 Washiriki wa shindano la Maisha Plus Msimu wa tano wakiwa wanaingia kijijini huku kila mmoja akiwa amefungwa kitambaa usoni wasijue wapo wapi.
Mwenyeji wa Kijiji Babu wa Maisha Plus akiwa anawakaribisha washiriki kwa namna yake
 Hapa Washiriki wakiendelea kuingia katika kijiji cha Maisha Plus huku wasifahamu wapo wapi.
 Masoud Kipanya akiwapa maelekezo washiriki wa Shindano la Maisha Plus kabla hawajafungua rasmi vitambaa na kujua wapo wapi
 Hivi ni Baadhi ya Vifaa na vitu ambavyo vijana wa Maisha Plus watakuwa wakivitumia kipindi wapo kijijini kwa Muda wa Wiki 8
 Masoud Kipanya akitoa msisitizo wa Jambo kwa washiriki wa shindano la Maisha Plus Msimu wa tano
Washiriki wa wa Shindano la Maisha Plus Msimu wa tano wakiwa wanafungua vitambaa kuona rasmi kijiji ambacho wataishi kwa wiki 8
Hapa ilikuwa ni kasheshe baada ya kufungua vitambaa na kukuta wapo porini sehemu wasiyo ijua huku kukiwa hakuna jengo lolote.
Hapa washiriki wa shindano la Maisha Plus wakiwa wanajipanga kuanza kufanya mchakato wa kuanza kujenga nyumba zao
Bado shughuli ilikuwa ni Pevu sana hawaelewi kabisa wanaanzia wapi wanaishia kujishauri kwanza huku kila mmoja akiwaza Tsh 30,000,000
Hapa bado shughuli ndio kwanza ilikuwa inaanza washiriki hawa pia walikuwa wakibadilishana mawazo wafanyeje.
Babu wa Kijiji cha Maisha Plus akiwa anatoa maelezo ya kina kwa washiriki wa shindano hilo ambao wanatoka katika Nchi 5 Afrika Mashariki jinsi gani wataishi, watakavyojenga nyumba zao na watakavyo ishi katika kijiji cha Maisha Plus
Wakiwa wanaleta mizigo yao ndani ya Kijiji cha Maisha Plus
Mmoja wa washiriki wa Shindano la Maisha Plus akinoa panga kwa ajili ya kujiandaa kwenda kukata miti kwa ajili ya kujenga nyumba zao za kuishi ambapo kila nyumba moja watakuwa wanaishi washiriki watatu.
Baadhi ya Mizigo ya washiriki baada ya kuwasili katika kijiji cha Maisha Plus
Washiriki wa Shindano la Maisha Plus wakiwa wameanza kuandaa makazi yao
Kazi Ikiendelea ya Kuandaa sehemu ya Kuishi
Hapa kazi tu yani kila mtu yupo na yake alimradi tuu wapate kujenga nyumba za kuishi katika kijiji hicho cha Maisha Plus.
Kulikuwa hakuna namna lazima kila mmoja afanye kazi ili wapate sehemu ya kulala
Wakati wenzake wamekwenda tafuta Miti ya Kujengea nyumba yeye alikuwa anatengeneza mpini
Babu wa Kijiji cha Maisha Plus akiwa anatoa maelekezo na kutoa vipimo vya jinsi watakavyojenga nyumba zao
Kila mshiriki akiwa ameshika nyenzo yake kwa ajili ya kujenga nyumba zao za kuishi
Kazi zinaendelea hapa na sasa ilikuwa ni mwendo wa kukata miti ili kuwahi kumaliza kujenga nyumba na kuanza kuishi.
Babu wa Maisha Plus akiwa anafatilia jambo kijijini hapo.
Bila kuchakalika na kazi ya kujiandaa kutafuta miti na kujenga nyumba unaweza kujikuta unalala nje
Baadhi yao walikuwa wamesha anza kuweka nguzo za nyumba zao
Akionekana akikomaa kuchimba kitu kabla hajawekea mpini
Ukiwa katika kijiji cha Maisha Plus  lazima uwe mbunifu sana .. hawa jamaa washiriki wa Shindano la Maisha Plus msimu wa 5 2016 wakiwa wanakata miti kwa ajili ya kujenga nyumba ambapo wataishi kwa wiki 8
Pori kwa pori
 Picha zote kwa hisani ya Fredy Njeje
Maisha Plus East Africa 2016 #HapaKaziTu #VijanaNdioNgazi